ENTERTAINMENT

Msanii wa injili Kenya afariki baada ya kuchomwa moto

Msanii wa muziki wa injili nchini Kenya, Rachel Wandeto, ameripotiwa kufariki dunia akiwa hospitalini baada ya kujeruhiwa vibaya katika tukio la kushambuliwa kwa kuchomwa moto kwa petroli lililotokea jijini Nairobi.

Rachel alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Kenyatta (KNH) ambapo alikuwa akipatiwa matibabu ya dharura kutokana na majeraha makubwa ya moto yaliyoathiri sehemu kubwa ya mwili wake.

Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali kutoka nchini Kenya, Wandeto alijulikana zaidi mitandaoni baada ya kuchora tatoo ya Rais wa Kenya William Ruto kama ishara ya kumuunga mkono kisiasa, jambo lililozua mjadala mkubwa na kumfanya kuwa gumzo katika mitandao ya kijamii na sehemu ya wananchi.

Inaelezwa kuwa alishambuliwa na watu wasiojulikana katika eneo la Mwiki, Kasarani jijini Nairobi, ambapo walimwagiwa petroli na kisha kumchoma moto kabla ya kutoroka. Jeshi la Polisi nchini Kenya linaendelea na uchunguzi kubaini chanzo na wahusika wa tukio hilo, huku viongozi, wasanii na mashabiki wakiendelea kutuma salamu za rambirambi kufuatia kifo chake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *