Gamondi ataja mambo mawili muhimu kwa Stars kuelekea Rwanda
Kocha wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Miguel Gamondi, amesema maandalizi ya kikosi cha Taifa Stars kuelekea mashindano ya FIFA Series nchini Rwanda yanalenga mambo makuu mawili; kujenga timu imara yenye ushindani na kuboresha kiwango cha wachezaji.
Gamondi alieleza kuwa maandalizi hayo yanahusisha kuimarisha mbinu za kiufundi, nidhamu ya wachezaji pamoja na mshikamano ndani ya kikosi ili kuhakikisha timu inakuwa katika hali nzuri ya ushindani.
Taifa Stars inatarajiwa kuanza kampeni yake Machi 26 kwa kucheza dhidi ya Liechtenstein, huku hatima ya mechi zinazofuata ikitegemea matokeo ya mchezo huo wa kwanza. (Mwanaspoti)
Endapo timu itashinda, itatinga hatua ya fainali, lakini ikipoteza italazimika kucheza mechi ya kusaka nafasi nyingine kulingana na matokeo ya michezo mingine.
Kocha huyo pia alikiri kuwa kulikuwa na changamoto katika kuchagua kikosi, lakini ana imani na wachezaji alio nao, akisisitiza ushindani ndani ya timu ni muhimu kwa maendeleo ya Taifa Stars kuelekea mashindano hayo ya kimataifa. (Mwanaspoti)
